Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:31

Jeshi la Ukraine laharibu ngome ya majeshi ya Russia katika mkoa wa Donetsk


Majeshi ya Ukraine yashambulia ngome ya Russia katika mji karibu na Bakhmut, mkoa wa Donetsk, Ukraine, July 2, 2023.
Majeshi ya Ukraine yashambulia ngome ya Russia katika mji karibu na Bakhmut, mkoa wa Donetsk, Ukraine, July 2, 2023.

Jeshi la Ukraine lilisema Jumanne limeharibu ngome ya majeshi ya Russia katika mkoa wa Donetsk huko mashariki mwa Ukraine.

Ukraine ilisema shambulizi hilo limetokea katika eneo linalokaliwa kimabavu na Russia la Makiivka.

Maafisa wa Russia walisema shambulizi la Ukraine liliua raia mmoja na kujeruhi wengine 36.

Ukraine na Russia zimeshutumiana kwamba kila upande unapanga kushambulia eneo linaloshikiliwa na Russia la kinu cha nishati ya nyuklia la Zaporizhzhia huko kusini mashariki mwa Ukraine.

Eneo hilo liko katika kitovu cha hofu katika mgogoro huo tangu Russia ilipokivamia Februari 2022.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya nyuklia limetahadharisha mara kadhaa kuhusu uwezekano wa kutokea maafa kutokana na mashambulizi ya mabomu yanayoendelea katika eneo hilo ambapo pande zote Russia na Ukraine zinalaumiana.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema amezungumza suala hilo kwa simu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

“Dunia lazima itambue hivi sasa kwamba usalama wa pamoja unategemea kikamilifu tahadhari ya ulimwengu kwa vitendo vya wavamizi katika kinu hicho cha nyuklia.

Russia lazima ielewe wazi kuwa dunia inashuhudia kile magaidi wanachopanga kutekeleza, na dunia iko tayari kujibu hilo,” Zelenskyy alisema katika hotuba ya Jumanne usiku.

Mionzi ya nyuklia ni tishio kwa kila mtu duniani, na kinu cha nishati ya nyuklia ni lazima kilindwe kikamilifu kisipate hali yoyote ya kuvuja kwa mionzi yake."

Some information for this story came from The Associated Press, Agence France-Presse and Reuters.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Tu

Forum

XS
SM
MD
LG