Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:12

Ukraine inasema imechukua tena kilomita mraba 37 mashariki na kusini mwa nchi


Wanajeshi wa Ukraine wasimama mbele ya jengo wakiwa na bendera ya taifa, katika operesheni ambayo ilikomboa kijiji cha kwanza katika mkoa wa Donetsk, Juni 11, 2023
Wanajeshi wa Ukraine wasimama mbele ya jengo wakiwa na bendera ya taifa, katika operesheni ambayo ilikomboa kijiji cha kwanza katika mkoa wa Donetsk, Juni 11, 2023

Ukraine Jumatatu imesema vikosi vyake vilichukua tena kilomita mraba 37 eneo la mashariki na kusini mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

Naibu waziri wa ulinzi Hanna Maliar alisema kwenye mtandao wa telegram kwamba wanajeshi wa Ukraine wanasonga mbele katika eneo la Bakhmut mashariki mwa nchi, huku Russia ikifanya mashambulizi katika maeneo ya Lyman, Adviika na Mariinka.

Maliar alisema mapigano makali yanaendelea katika maeneo hayo.

Maliar alisema maeneo mengi yaliyochukuliwa yanapatikana kusini mwa nchi, ambapo kilomita mraba 28 zilichukuliwa tena wiki iliyopita. Aliongeza kuwa jeshi la Ukraine limekua likiendesha operesheni za mashambulizi katika maeneo ya Melitopol na Berdyansk.

Ukraine mapema mwezi Juni ilianzisha mashambulizi ya kuchukua tena maeneo yanayodhibitiwa na Russia tangu ilipoanzisha uvamizi wake dhidi ya Ukraine mwezi Februari mwaka wa 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG