Kundi la kwanza la wahamiaji kutoka Uingereza linatarajiwa kuwasili nchini Rwanda katika wiki za karibuni.
Hii inafuatia tangazo la serikali ya Uingereza kuingia makubaliano na serikali ya Rwanda kuwapokea baadhi ya wahamiaji kutoka Ufaransa wanaoingia Uingereza kwa kutumia boti chakavu au malori ya kubeba mizigo.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kwamba hatua hiyo itaokoa maisha ya watu wengi na kufikisha kikomo magendo ya usafirishaji watu.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa hatua hiyo wakisema kwamba inakiuka haki za kibinadamu.
Mpango huo ni mbinu ya kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Uingereza.