Uingereza imeingia makubaliano na Rwanda kuwahamisha baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi kwenda katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Serikali ya Rwanda itapokea malipo ya awali ya dola milioni 150 kushiriki katika mpango huo.
Waziri Mkuu Boris Johnson amekuwa akitoa maelezo ya mpango huo ambao utawafanya wanaume wasio na wake wanaoomba hadhi ya ukimbizi kupelekwa umbali wa kilomita 6,000 ili kupata makazi mapya nchini Rwanda.
Anasema anachukua hatua kuwazuia watu wanaofanya magendo. Serikali ya Uingereza iko katika shinikizo kuzuia maelfu ya watu kufanya safari hatari kuelekea kusini mwa Uingereza kwa kutumia boti ndogo.
Mashirika ya kutoa misaada yamelaani mpango huo wa kuwahamisha watu kama ukatili na kuelezea wasiwasi wao kuhusu rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Rwanda.