Nekkaz anayetaka kugombea nafasi ya urais dhidi ya Bouteflika katika uchaguzi April 18, 2019, nchini humo amesema alikwenda katika hospitali kutaka kujua zaidi kuhusu Matibabu ya rais huyo wa Algeria mwenye umri wa miaka 82 yanavyoendelea, vyanzo vya habari vimeeleza.
Pia aliandaa maandamano madogo nje ya hospitali hiyo kabla ya kutaka kuingia ndani.
Msemaji wa polisi Jijini Geneva, Jean-Philippe Brandt amethibitisha kukamatwa kwa Rachid Nekkaz na amesema anatarajiwa kukabidhiwa kwa mwendesha mashtaka Jumamosi.
Rais Bouteflika, aliyeko madarakani tangu mwaka 1999, hajaonekana hadharani tangu alipougua kiharusi mwaka 2013.
Azma yake ya kutaka kuwania muhula wa tano katika uchaguzi wa Algeria imesababisha maandamano makubwa ndani na nje ya nchi hiyo yakoongozwa na vijana wanaomtaka Bouteflika kuondoka madarakani.
Maandamano kwa sehemu kubwa yamefanyika katika hali ya amani lakini yale ya Ijumaa wiki iliyopita yanayosemekana yalikuwa makubwa kabisa, kulikuwepo na ripoti za ghasia zilizosababisha mtu mmoja kuuawa na karibu 40 kujeruhiwa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC