Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:35

Ahadi mpya ya Bouteflika kwa wananchi wa Algeria


Wanafunzi wakikabiliana na askari wa kuzuia fujo nchini Algeria
Wanafunzi wakikabiliana na askari wa kuzuia fujo nchini Algeria

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ameahidi siku ya Jumapili hatakamilisha muhula kamili wa miaka mitano akichaguliwa tena wakati wa uchaguzi wa mwezi Aprili.

Wachambuzi wanasema uamuzi huo ni juhudi za kuwaridhisha waandamanaji kote nchini wanaomtaka asigombee tena kiti cha urais baada ya miaka 20 ya utawala wake.

Maandamano yaliyoanza siku 12 zilizopita katika chuo kikuu cha Algiers yameenea kote nchini na katika miji kadhaa ya ufaransa na nchi jirani kumtaka kiongozi huyo ajiengua kutoka madarakani.

Bouteflika azuru Geneva

Rais Abdelaziz Bouteflika alifika Geneva Uswisi wiki moja iliyopita kwa kile ofisi yake inachokieleza kwenda kupimwa afya yake, lakini gazeti la Geneva La Tribune la Geneva likinukuu duru kadhaa linathibitisha kwamba kiongozi huyo anatibiwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Geneva, HUG.

Kutokana na hayo ni mkurugenzi wake wa kampeni Abdelghani ndiye aliyewasilisha rasmi maombi yake ya kushiriki katika uchaguzi wa Aprili 18 hapo usiku wa manane, ambayo ni siku ya mwisho kujiandikisha wagombea kiti cha urais.

Mgombea alipata kiharusi

Kiongozi huyo asiyeonekana sana hadharani alipata kiharusi mwaka 2013 na baadae mshtuko wa moyo na tangu hapo yuko kwenye kiti cha mgonjwa aliahidi kwamba ataitisha mkutano wa kitaifa na uchaguzi wa mapema baada ya mwaka mmoja, ambao hatashiriki. Baada ya kuwasilisha hati za kushiriki katika uchaguzi, Mkurugenzi wa kampeni ya Boutflika, Abdelghani Zaalane alikuwa na haya yakusema:

"Nina ahidi kutayariusha mara moja baada ya uchaguzi wa rais mkutano wa kitaifa utakao kiuwa huru na kuwahusisha kila mtu, ili kujadili, kutayarisha na kuishinisha mageuzi ya kiuchumi kijami na vyombo vya utawala yatakayo kuwa msingi wa mfumo mpya utakao fufua maendeleo ya Algeria."

Ahadi ya rais kutogombea tena

Ahadi ya Bouteflika ilitolewa baada ya maandamano yaliyoanzishwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Algeria hapo Februari 22 wakiimba Bouteflika lazima aondoke hatutaki muhula wa tano.

Hivi sasa maandamano yameenea kote nchini na ufaransa ambapo waandamanaji wanasema wamechoshwa na utawala wa chama kimoja cha FNL tangu uhuru wa Algeria 1962.

Maoni ya raia wa Algeria

Fatima Bendaoud-bouda mkurugenzi wa shule anasema ni lazima kwa wazee wote katika ofisi ya rais waondoke.

Fatima Bendaoud-Bouda ameongeza :

"Kuna mamia ya watu wanaume na wanawake wenye uwezo wa kuchukua madaraka. Kile watu wanachotaka sasa hivi, ambacho kitakuwa kizuri ni kuundwa baraza litakalochaguliwa na wananchi kuwakilisha vuguvugu hili letu na kuondowa kabisa mfumo wa utawala uliyoko."

Maandamano yanaongozwa na wanafunzi na kutaka mabadiliko hayo kwa vile upinzani uko dhaifu na umegawika na wachambuzi wanasema hawawezi kuleta ushindani mkubwa kwa Bouteflika.

Hadi hivi sasa kuna wagombea 6 walokwisha jiandikisha miongoni mwao mfanya biashara Nezzaz anaeungwa mkono na vijana

Rachid Nezzaz Mfanya biashara mgombea kiti cha rais amesema :

Tusiwe na wasi wasi , ni lazime tuonyeshe mandhari nzuri ya Algeria na demokrasia ya Algeria. Kuhusiana na rais munafahamu sina tatizo na Rais Buteflika ambaye hadi april 18 atakuwa rais wa Algeria.

Algeria haikuguswa na maandamano makubwa ya nchi za kiarabu ya 2011, lakini safari hii maandamano yameenea hadi Ufransa na nchi jirani ya Tunisia ambako jana maandamano makubwa yalishuhudiwa, waandamanaji wakibeba mabango na bendera ya taifa wakipinga muhula wa tano kwa Bouteflika .

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG