Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:44

Wananchi Algeria waendelea kupinga Bouteflika kushiriki uchaguzi 2019


Mamia ya wanafunzi wakusanyika katikati ya jiji la Algiers tayari kuandamana kupiga Rais Abdelaziz Bouteflika kuwania awamu ya tano ya urais, Jumanne , Machi 6, 2019.
Mamia ya wanafunzi wakusanyika katikati ya jiji la Algiers tayari kuandamana kupiga Rais Abdelaziz Bouteflika kuwania awamu ya tano ya urais, Jumanne , Machi 6, 2019.

Maandamano ya kupinga serikali yameendelea huko Algeria Jumatano wakati Rais Abdelazizi Bouteflika anasubiriwa kutangaza rasmi anagombea muhula wake wa tano.

Wakati hilo likisubiriwa na wananchi wa Algeria kabla ya muda wa mwisho wa kujiandikisha kugota usiku wa manane Alhamisi.

Bouteflika aliyemadarakani tangu 1999 alielekea Uswisi Jumatano jioni kwa kile ofisi yake inaeleza amekwenda kufanyiwa vipimo vya kawaida kujua hali yake ya kiafya.

Kwa mujibu wa serikali ya Algeria sheria ya nchi hiyo haimhitaji mtu kuwepo nchini kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa mwezi April.

Maandamano katika barabara za miji mbalimbali ya Algeria yalianza karibu siku10 zilizopita wakati Bouteflika alipotangaza nia yake ya kugombania kwa muhula wa tano.

Maandamano kwa sehemu kubwa yamefanyika katika hali ya amani lakini yale ya Ijumaa yanayosemekana yalikuwa makubwa kabisa kulikuwepo na ripoti za ghasia zilizosababisha mtu mmoja kuuawa na karibu 40 kujeruhiwa.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kwa muda mrefu hajaonekana hadharani na anatumia kiti cha mgonjwa tangu alipopatwa na kiharusi 2013.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG