Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:52

Kiongozi wa Kikurdi Syria ampongeza Rais mteule Biden na makamu wake


Jeneral Kamanda Mazloum Abdi
Jeneral Kamanda Mazloum Abdi

Kiongozi wa Kikurdi nchini Syria amezungumzia azma ya kuendeleza ushirikiano na Marekani kwa msaada wake kwa vikosi vyake,

Kauli hii imekuja baada ya kutangazwa mshindi Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa wiki iliyopita.

Vikosi vya kikurdi vya Syrian Democratc Forces – SDF – vimekuwa na ushirika na Marekani kwa kiwango kikubwa katika kupambana na kundi la kigaidi la Islamic State.

Vikosi hivyo vinaungwa mkono na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kupambana na Islamic State.

Wapiganaji wa SDF wamekomboa himaya nyingi ambazo zilikuwa zikishikiliwa na wanamgambo wa IS nchini Syria.

Mazloum Abdi, Jenerali Kamanda wa SDF, amempongeza Joe Biden kuchaguliwa kuwa Rais mteule wa Marekani, na kumpongeza makamu wake mteule Kamala Harris.Islam

XS
SM
MD
LG