Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:45

Raia wa Uingereza aliyejiunga na IS Syria apokonywa uraia


Kadiza Sultana, 16, kushoto, Shamima Begum,15, katikati 15-year-old Amira Abase, 15, walipokuwa wanapita uwanjwa wa ndege wa Gatwick, Uingereza
Kadiza Sultana, 16, kushoto, Shamima Begum,15, katikati 15-year-old Amira Abase, 15, walipokuwa wanapita uwanjwa wa ndege wa Gatwick, Uingereza

Wakili wa familia ya Shamima Begum, msichana aliyetoroka nyumbani kwao London, Uingereza miaka minne iliyopita akiwa na umri wa miaka 15 na kujiunga na kundi la Islamic State, anasema serikali ya Uingereza imempokonya uraia wake.

Familia yake inaeleza kwamba imesikitishwa na uamuzi huo na inatafakari juu ya hatua zote za kisheria kupinga uwamuzi huo.Begum, ni mmoja wa vijana wa Uingereza aliyejiunga na IS.

Shamima Begum mwenye umri wa miaka 19 hivi sasa akiwa amezaa mtoto wake wa tatu mwishoni mwa wiki anasema anataka kurudi nyumbani.

Alipohojiwa na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Sky kwenye kambi inayoshikiliwa hivi sasa na kundi la Wakurdi wanaosaidiwa na Marekani huko Syria, ikiwa anafahamu kuna mjadala mkali Uingereza wa iwapo aruhuiswe kurudi nyumbani, Shamima alisema anafahamu.

Ninadhani watu wengi inabidi kunionea huruma kutokana na matatizo yaliyonikuta, unajuwa, sikufahamu kile nilichokuwa ninafanya nilipoondoka. Kwa hiyo ninamatumaini kwa sababu yangu kwa sababu ya mtoto wangu wataniruhusu nirudi nyumbani. Kwa sababu siwezi kuendelea kuishi katika kambi hii.

Shamima alikimbia pamoja na wanafunzi wenzake watatu na mmoja aliuawa kutokana na shambulio la bomu na watoto wake wawili walifariki kutokana na maradhi.

Wakili wa familia yake Begum, Mohammed Akunjee akizungumza na kituo cha tekevisheni Sky anasema wanafanya kila wawezalo ili wamrudishe nyumbani.

Mohammed Akunjee wakili wa familia ya Begum amesema : "Tuna matumaini kwamba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza itaweza kutoa hati ya kusafiri kwa mtoto na mjukuu wao ambaye hana hatia yeyote. tunaomba warudishwe nyumbani halafu wachukuliwe hatua za kisheria kulingana na sheria za Uingereza.

Lakini hali hiyo inaonekana hivi sasa itakuwa ni ngumu kwani Waingereza wengi hawataki vijana waliyokimbia na kujiunga na wapiganaji wa itikadi kali kurudi nyumbani. Inakadiriwa kuna vijana karibu 900 wa Uingereza waliyoenda Syria na Iraq kujiunga na ISIS.

Mbunge wa upinzani Bunge la Uingereza Lord Charlile anasema Waziri wa Mambo ya Ndani Sajid Javid anachukuwa hatua za kisheria ikiwa atampokonya uraia wake.

Lord Carlile mbunge wa upinzani baraza la Lords Uingereza amesema : "Ndio Waziri wa Mambo ya Ndani ameeleza bayana mawazo yake mara tu kasheshe hii ilipozuka na amekuwa na msimamo moja. Ninadhani kutakuwepo na mchanganyiko wa hisia lakini ninadhani idadi kubwa ya waingereaza hawamtaki hasa Begum kurudi nchini."

Kawaida Muingereza hapokonywi uraia wake ikiwa hana uraia wa nchi nyingine. Lakini Begum inaaminika anaweza kupata uraia wa Bangladesh kupitia mama yake.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud

XS
SM
MD
LG