Meja Jenerali Rupert Jones wa jeshi la Uingereza amewaambia wanahabari kuwa vikosi vya Iraq vinaenda nyumba hadi nyumba kuwatokomeza wapiganaji waliobaki Mosul, mji ambao Islamic State iliuteka miaka 3 iliopita.
Jones pia amesema kuwa kuanguka kwa makao makuu ya mji wa Raqqa nchini Syria ambayo ni makao makuu ya Kikundi cha IS, “ni kitu kinasubiri wakati wake ufike,” lakini akatahadharisha kuwa vita hiyo sio nyepesi au itamalazika haraka.
Vikosi vya Iraq vikisaidiwa na mashambulizi ya anga kutoka kwa muungano vilipenya ndani zaidi ya mji wa Mosul Jumapili wakati kamanda mmoja wa Iraq akisdema kuwa asilimia 65 hadi 70 ya mji huo imechukuliwa tena.