Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:55

Kiongozi wa dhehebu lisilo rasmi ashitakiwa kwa tuhuma za mauaji ya watoto Kenya


Kiongozi wa dhehebu lisilo rasmi Paul Nthenge Mackenzie alipokuwa katika kahakama ya Malindi Januari 17 2024. Picha na AFP.
Kiongozi wa dhehebu lisilo rasmi Paul Nthenge Mackenzie alipokuwa katika kahakama ya Malindi Januari 17 2024. Picha na AFP.

Kiongozi wa dhehebu lisilo rasmi, Paul Mackenzie na waumini wengine 29 wameshitakiwa leo kwa mauaji ya watoto 191 ambao miili yao ilikutwa miongoni mwa idadi ya watu wengine mara mbili zaidi waliozikwa katika msitu.

Washitakiwa wote wamekana mashitaka yaliyofikishwa mbele ya mahakama katika mji wa mwambao wa Malindi. Ilibainika kuwa mtuhumiwa mmoja hakuwa na akili nzuri kuweza kukabiliana na mashitaka hayo.

Waendesha mashitaka wamesema Mackenzie aliamuru wafuasi wake kujinyima kula chakula na watoto wao hadi kufa ili waweze kufika mbinguni kabla ya dunia haijaisha , katika moja ya majanga mabaya ya ushawishi wa Imani potofu katika historia ya karibuni.

Makenzie alikamatwa April mwaka jana. Tayari alishitakiwa na uhalifu unaohusiana na ugaidi, mauaji ya watu bila kukusudia na mateso. Makenzie pia alikutwa na hatia mwezi Desemba kwa kutengeneza filamu bila kuwa na leseni na kuhukumiwa miezi 12 jela.

Forum

XS
SM
MD
LG