Lori lililokuwa limebeba mitungi ya gesi lilipuka kabla ya saa sita usiku siku ya Alhamisi huko Embakasi, wilaya moja katika mji mkuu wa Nairobi yenye wakazi wengi, na kusababisha uharibifu mkubwa na kupelekea watu kukimbia ili kunusuru maisha yao.
Taasisi ya Petroli ya Afrika Mashariki ilisema Ijumaa kwamba mlipuko huo ulitokea kwenye ghala haramu ya kujazia na kuhifadhi mafuta, ambako mmliki wake na baadhi ya wateja walikutwa na hatia na kuhukumiwa mwezi Mei mwaka 2023.
Lakini Mamlaka ya Mazingira Kenya (NEMA) imesema Jumamosi kwamba kampuni ya nishati Maxxis Nairobi Energy ilipata leseni tarehe 2 Februari mwaka jana kusimamia ghala hiyo.
“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa maafisa wanne wa NEMA walitoa leseni bila kuheshimu taratibu na kwa hiyo wana hatia,” mwenyekiti wa bodi ya NEMA Emilio Mugo amesema katika taarifa.
Forum