Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:37

Kinyang'anyiro cha urais Kenya, takwimu zaonyesha kiko sawa


Konza, Kenya
Konza, Kenya

Kura mpya ya maoni ya shirika la utafiti la Tifa lenye makao yake  mjini Nairobi inaonyesha kuwa kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa Kenya kiko sawa ki takwimu.

Raila Odinga kiongozi wa upinzani anayewania nafasi hiyo kwa mara ya tano, anaongoza kwa asilimia 46.7 na mpinzani wake William Ruto naibu rais wa sasa ana asilimia 44.4 ya kura.

Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ili kushinda katika duru ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu, mgombea ana hitaji zaidi ya nusu ya kura zote angalau asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo takriban nusu miongoni mwa yote 47.

Ikilinganishwa na kura za maoni za awali za utafiti wa Tifa, sasa zinaonyesha kuwa kura za Dr Ruto amepunguza idadi ya dhidi ya Raila Odinga ambaye awali alikuwa na asilimia 42 dhidi ya asilimia 39 za ruto.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa Odinga ana uungwaji mkono zaidi katika maeneo ya Nyanza , magharibi ya Kusini ya Rift, Nairobi na sehemu za Lower Eastern, wakati Dr Ruto ana uungwaji mkono zaidi katika maeneo ya kati ya Rift na Mlima Kenya .

XS
SM
MD
LG