Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:56

Hongo kwa wapiga kura yasababisha uhaba wa noti ndogo ndogo kwenye benki za kenya-Matiang'i


Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i

Benki za Kenya zinakabiliwa na uhaba wa noti ndogo ndogo kwa sababu wanasiasa wanawapa hongo raia kujaribu kupata kura zao kwenye uchaguzi wa mwezi ujao, waziri ma mambo ya ndani ametoa tuhuma hizo Jumatano.

Wanasiasa wamekuwa wakitoa kiasi kidogo cha pesa taslimu au vitu vingine vya bure kwa watu wanaojitokeza kwenye mikutano yao ya kampeni kabla ya uchaguzi wa Agosti 9 katika nchi hiyo ambako ufisadi umekithiri.

“Utawaona watu wakibeba pesa kwenye mifuko, wakiwapanga raia na kuwapa shilingi 200,” waziri Fred Matiang’i amesema.

“Kuna uhaba wa noti za shilingi 200 katika benki na noti za shilingi 100 katika benki zenu kwa sababu wanasiasa wanawahonga wanavijiji,” amewambia waandishi wa habari wakati wa kikao kifupi kuhusu utakatishaji wa fedha na ugaidi.

Hata hivyo kutoa hongo ni kosa la uvunjaji wa sheria za uchaguzi linaloadhibiwa kwa faini ya hadi shilingi milioni 2, sawa na dola 17,000, au kifungo cha miaka sita jela.

Mwezi ujao, Wakenya watamchagua sio tu rais mpya lakini pia mamia ya wabunge na wawakilishi wapatao 1,500 wa kaunti.

XS
SM
MD
LG