Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:18

Kenya: Mwili wa Edwin Chiloba wapatikana ukiwa umefungwa ndani ya sanduku


Edwin Chiloba
Edwin Chiloba

Polisi nchini Kenya wameupata mwili wa Edwin Chiloba, mwanaharakati maarufu anayetetea  mapenzi ya jinsia moja, ukiwa umefungwa ndani ya sanduku la chuma huko magharibi mwa Kenya, vyombo vya habari  vya Kenya vimeripoti Ijumaa.

Abiria wa bodaboda walitoa taarifa kwa polisi baada ya kuona sanduku limetupwa kando ya barabara kutoka kwenye gari ambalo namba za usajili zilizibwa, magazeti ya "The Standard "na "The Daily Nation" yameripoti yakikariri vyanzo vya polisi.

Mwili wa Edwin uligundulika Jumanne karibu na mji wa Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu, ambako alikuwa anaendesha biashara zake za mitindo, Iimesema kundi huru la kutetea, Kenya Human Rights Commission (KHRC).

“Ameuwawa kikatili na kutupwa na watu washambuliaji wasio julikana,”KHRC wamesema kupitia mtandao wa Twitter.

Kweli inatia wasiwasi kwamba tunaendelea kushuhudia ongezeko la ghasia zinazowalenga watu walio katika mapenzi ya jinsia Kenya.

Utafiti unaonyesha kuna ongezeko la kukubalika kwa watu wa jamii hiyo nchini Kenya, lakini wengi bado wanawaona wanakwenda kinyume na maadili. Miaka ya karibuni, Tume ya taifa ya filamu ilipiga marufuku uonyeshwaji wa filamu mbili zenye taswira za maisha ya watu walio katika mapenzi ya jinsia moja.

Msemaji wa polisi nchini Kenya, Resila Onyango amesema atalizungumzia suala hili baadaye, wakati Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu , Ayub Gitonga Ali amekataa kutoa e .

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG