Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 20:37

Keir Starmer ndiye Waziri Mkuu mpya wa Uingereza


Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer.
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer.

Uingereza ina Waziri mkuu mpya. Keir Starmer  anakuwa Waziri mkuu wa 58 wa taifa hilo, ambapo chama chake cha  Leba kinarejea tena mamlakani baada ya zaidi ya mwongo mmoja kama upinzani, kufuatia ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi nchini humo.

Hii ni licha ya wapiga kura kuonyesha kuchoshwa na siasa.

Chama hicho sasa kina kibarua kigumu cha kufufua uchumi uliodumaa, katika taifa ambalo limevunjika moyo.

Kiongozi wa chama hicho, Keir Starmer, anakuwa Waziri mkuu mpya, akikiongoza kurejea madarakani, takriban miaka mitano baada ya kupata pigo kubwa zaidi kisiasa, katika kipindi cha takriban karne moja.

Starmer atachukua usukani baada ya Waziri mkuu anayeondoka Riki Sunak, kuwasilisha waraka wake wa kujiuzulu kwa Mfalme Charles.

Sunak tayari amekiri kushindwa, na kusema kwamba anawajibika kwa matokeo hayo ya uchaguzi.

“Naondoka kwa kazi hii, kwa heshima, baada ya kuongoza nchi bora zaidi duniani,” alisema Sunak, katika hotuba yake ya mwisho nje ya makao yake rasmi ya 10 Downing Street.

Huku karibu kura zote zikiwa zimehesabiwa, chama cha leba kimeshinda viti 410 katika baraza la chini la bunge, huku kile cha Konsevativ kikipata viti 118 kati ya vyote 650.

Forum

XS
SM
MD
LG