Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 07, 2024 Local time: 09:14

Zoezi la Uchaguzi laanza Uingereza Alhamisi


Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak

Wapiga kura wa Uingereza leo Alhamisi wameshiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao kwa kiasi kikubwa unatarajiwa kutoa ushindi kwa chama cha upinzani cha Labour, na kumaliza utawala wa karibu muongo mmoja na nusu wa utawala wa chama cha Conservative.

Huu ni uchaguzi wa kwanza wa kitaifa tangu Boris Johnson aliposhinda kwa wingi hapo 2019, na ambao umeitishwa na waziri mkuu Rishi Sunak, miezi 6 kabla ya tarehe iliyopangwa. Mpango huo huenda ukaenda kinyume na yeye kwa kuwa kura za maoni wakati wa kipindi cha wiki 6 za kampeni, pamoja na zile za miaka miwili iliyopita zinaonyesha kushindwa vibaya kwa chama chake cha mrengo wa kulia.

Hali hiyo huenda ikamuweka kiongozi wa Labour Keir Starmer, mwenye umri wa miaka 61 ofisini, huko Downing Street, kama kiongozi wa chama chenye wingi katika bunge. Upigaji kura ulianza saa moja za asubuhi, kwenye zaidi ya vituo 40,000 vya kupigia kura kote nchini, kwenye kumbi za kanisa, kumbi za kijamii, shule pamoja na maeneo yasio ya kawaida kama vile vilabu na kwenye meli.

Sunak alikuwa miongoni mwa wapigaji kura wa kwanza kwenye eneo lake la uwakilishi bungeni la Richmond na Northallerton, jimboni Yorkshire, kaskazini mwa Uingereza. Starmer alipiga kura takriban saa mbili baadaye mjini London.

Forum

XS
SM
MD
LG