Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 11:03

Chama cha Labor chatabiriwa ushindi Uingereza


Kiongozi wa Chama Cha Labor, Keir Starmer akifanya kampeni huko Redditch Worcestershir, Julai 3, 2024. Picha na Reuters.
Kiongozi wa Chama Cha Labor, Keir Starmer akifanya kampeni huko Redditch Worcestershir, Julai 3, 2024. Picha na Reuters.

Chama cha Labour nchini Uingereza kinaelekea kupata ushindi dhidi ya chama tawala cha Conservative cha Waziri Mkuu Rishi Sunak baada ya miaka 14 ya misukomisuko mingi.

Uksuanyaji maoni unakiweka chama cha Starmer cha mrengo wa kushoto kwenye mwelekeo wa kupata ushindi mkubwa lakini pia yanapendekeza kuwa wapiga kura wengi wanataka mabadiliko baada ya malumbano ya ndani na mivutano chini ya uongozi wa Conservatives ambao umepelekea kushuhudia mawaziri wakuu watano katika kipindi cha miaka minane.

Hii ina maana Starmer, mwenye umri wa miaka 61 wakili wa zamani wa haki za binadamu, huenda akachukua moja ya orodha ndefu ya mambo ya kufanya katika historia ya Uingereza uungaji mkono au rasilimali za kifedha kukabiliana nazo.

“Hivi leo Uingereza inaweza kuanza ukurasa mpya,” Starmer aliwaambia wapiga kura katika taarifa yake ya Alhamisi.
Hatuwezi kumudu miaka mingine mitano chini ya utawala wa Conservatives. Lakini mabadiliko yatatokea tu kama mtakipigia kura chama cha Labour.”

Forum

XS
SM
MD
LG