Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 06, 2024 Local time: 10:06

Uingereza: Chama kinachotawala kimekubali kwamba kitashindwa


Kiongozi wa chama cha Labour Keir Starmer (kushoto) katika mdahalo na waziri mkuu ambaye ni kiongozi wa chama cha Conservative Rishi Sunak. June 26, 2024
Kiongozi wa chama cha Labour Keir Starmer (kushoto) katika mdahalo na waziri mkuu ambaye ni kiongozi wa chama cha Conservative Rishi Sunak. June 26, 2024

Chama tawala nchini Uingereza, cha Conservative, kimekubali kwamba kitashindwa na chama cha upinzani cha Leba cha Keir Starmer, siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.

Conservative kimesema kwamba upinzani unelekea kupata ushindi wa kihistoria.

Kura za maoni zinaonyesha kwamba Leba kitapata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa kesho alhamisi na kufikisha kikomo utawala wa miaka 14 wa conservative, na kumfanya Starmer kuwa waziri mkuu.

Starmer na waziri mkuu Rishi Sunak, wamefanya kampeni ya mwisho kabla ya vituo vya kupiga kura kufunguliwa. Kila upande umeonya wapiga kura dhidi ya kumchagua mpinzani kwa msingi kwamba atavuruga uchumi wa Uingereza.

Conservatives wamesema wanastahili kuwashawishi wapiga kura ili kupata idadi ya kutosha ya wabunge ili kuwe na upinzani wenye nguvu bungeni.

Ukusanyaji wa maoni uliofanywa na Survation, unaonyesha kwamba chama cha Leba kitapata viti 484 kati ya viti 650 vya bunge. Idadi hiyo ni ya juu zaidi kuliko ya ushindi wa kishindo wa mwaka 1997 wa viti 418 chini ya uongozi wa Tony Blair.

Chama cha Conservative kimetabiriwa kupata viti 64 pekee, ikiwa ni idadi ndogo sana ya viti kwa chama hicho tangu mwaka 1834

Forum

XS
SM
MD
LG