Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:20

Rwanda yasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) lilidanganya mahakama ya Uingereza


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa 10 Downing Street, katikati mwa London, Mei 4, 2023. Picha na Stefan Rousseau / POOL/ AFP.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa 10 Downing Street, katikati mwa London, Mei 4, 2023. Picha na Stefan Rousseau / POOL/ AFP.

Rwanda ilisema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) lilidanganya lilipoiambia mahakama ya Uingereza wiki hii kwamba waomba hifadhi waliopelekwa katika nchi hiyo wanaweza kuhamishwa tena katika nchi  ambazo wanakabiliwa na hatari ya kuteswa au kuuawa.

Mawakili wanaoliwakilisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) walisema Jumatatu kuwa mfumo wa hifadhi ya Rwanda una mapungufu, kama sehemu ya changamoto kwa sera ya serikali ya Uingereza ya kuwafukuza wanaotafuta hifadhi huko.

Mawakili hao walisema sera hiyo inahatarisha wanaotafuta hifadhi kukabiliwa na mchakato uliopigwa marufuku unaojulikana kama wa kuwarudisha wakimbizi sehemu ambazo wanaweza kuteswa kwa kuzingatia ushahidi wa siku za nyuma ambao ulikuwa sehemu muhimu ya hoja ya Mahakama ya Juu ya Uingereza ilipotoa uamuzi wa mpango wa nchi hiyo kuwa kinyume cha sheria mwaka jana.

"UNHCR inadanganya," msemaji wa serikali ya Rwanda alisema katika taarifa yake siku ya Jumanne.

"Shirika hilo linaonekana kudhamiria kuwasilisha madai ya uwongo kwa mahakama za Uingereza kuhusu Rwanda inavyowahudumia waomba hifadhi, huku likiendelea kushirikiana nasi kuwaleta wahamiaji wa Kiafrika kutoka Libya kwenye usalama nchini Rwanda."

Forum

XS
SM
MD
LG