Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:19

Kampuni ya NetBlocks yasema Serikali ya Ethiopia yadhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Matumizi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii yamedhibitiwa nchini Ethiopia, kampuni binafsi inayofuatilia intaneti, NetBlocks ilisema, kufuatia maandamano ya ghasia yaliyozuka kutokana na mivutano ndaniya kanisa la Orthodox nchini humo.

Maandamano hayo yalizuka katika mkoa wa Oromiya wakati maafisa watatu wa kanisa walipojitangaza ni maaskofu mwezi uliopita na kuweka kanuni zao wa uongozi. Baadhi ya waandamanaji wamepinga hatua yao huku wengine wakiunga mkono.

Tangu maandamano yaanze tarehe 4 Februari, watu wasiopungua 30 wameuawa, taarifa ya kanisa hilo ilisema Alhamisi.

Taarifa hiyo iliitisha maandamano siku ya Jumapili, ikiishutumu serikali ya Ethiopia kwa "kuingilia" masuala ya ndani ya kanisa baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuwataka mawaziri wake kujiweka kando na mzozo huo.

Serikali ya Ethiopia imekuwa na utamaduni wa kudumisha uhusiano wa karibu na Kanisa la Orthodox, ambapo zaidi ya asilimia 40 ya wananchi ni waumini wa kanisa hilo.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia Legesse Tulu hakuweza kujibu mara moja maswali hususiana na suala hilo siku ya Ijumaa, lakini taarifa ya serikali ya Alhamisi ilisema maandamano yamepigwa marufuku ili kuzuia ghasia.

Matumizi ya Facebook, Messenger, TikTok na Telegram yamedhibitiwa vikali, NetBlocks ilisema katika taarifa ya Alhamisi jioni, ikizungumzia data wa mitandao walizokusanya.

Awali mamlaka za Ethiopia zilifunga au kudhibiti matumizi ya mitandao wakati wa machafuko ya kisiasa, yakiwemo maandamano ya mwaka 2020 ambapo mwimbaji maarufu kutoka Oromiya aliuwawa.

Chanzo cha taarifa hii inatoka Shirila la Habari la Reuters

XS
SM
MD
LG