Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 01, 2025 Local time: 22:53

Japan: Marufuku ya ndoa ya jinsia moja licha ya kufuata katiba yaibua wasiwasi kuhusu hadhi na haki za binadamu


Wanaounga mkono ndoa ya jinsia moja wakiandamana Tokyo, Japan, Wednesday, Nov. 30, 2022.
Wanaounga mkono ndoa ya jinsia moja wakiandamana Tokyo, Japan, Wednesday, Nov. 30, 2022.

Mahakama moja ya Japan siku ya Alhamisi ilisema marufuku ya ndoa za jinsia moja inafuatana na katiba lakini iliibua wasiwasi kuhusu hadhi na haki za binadamu za wapenzi wa jinsia moja.

Kulingana na vyanzo vya habari uamuzi huo ulikuwa na mapungufu kwa matarajio ya wanaharakati, lakini bado unaonekana kama hatua ya kusonga mbele.

Hukumu ya mahakama ya wilaya ya Fukuoka ilitolewa wiki moja baada ya mahakama nyingine ya wilaya kusema ni kinyume cha katiba kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.

Hukumu hiyo iliongeza matumaini ya mabadiliko miongoni mwa jumuiya ya LGBTQ nchini Japan, ambalo ni taifa pekee la nchi saba kuu duniani ambalo halina sheria ya kuwalinda watu wa ndoa za jinsia moja.

Maamuzi matano kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja yametolewa nchini Japan katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mawili yakihitimisha kwamba marufuku hayo yalikuwa kinyume na katiba, moja ikisema sivyo, na mawili, ikiwa ni pamoja na la Alhamisi, yakiunga mkono marufuku hiyo lakini kuibua masuala mengine ya haki

Mahakama ya Tokyo mwaka jana iliidhinisha marufuku hayo lakini ilisema ukosefu wa ulinzi wa kisheria kwa familia za jinsia moja ulikiuka haki zao.

Forum

XS
SM
MD
LG