Kustaafu kwa Breyer mwenye umri wa miaka 83, mmoja wa majaji wa kiliberali wa mahakama hiyo kutatoa nafasi ya kujaza kiti kilichokuwa wazi tangu rais wa zamani Donald Trump alipoteuwa wa-consevative watatu ambao walibadilisha usawa wa kiitikadi wa mahakama hiyo kwa mrengo wa kulia kwa wingi wa 6-3.
Biden bado hajatoa orodha ya majaji ambao anafikiria kuwateua kwa ajili ya nafasi hiyo katika mahakama yenye wajumbe tisa.
Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki amewaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa rais atafuata ahadi zake wakati wa kampeni kuchagua mwanamke wa kwanza mweusi katika Mahakama.
Psaki amesema: Ameteuwa idadi ya kihistoria ya majajji ambao ni watu wa rangi, sijui kama ni idadi ya kihistoria kwa wanawake, lakini majaji wengi aliowateuwa ni wanawake. Hii inaonyesha azma yake ya kutaka kuwa na mahakama kote nchini zinazo onekana kama Marekani, na hiyo inaonyesha uzoefu wa Marekani, ikiwemo watetezi wa umma na wengine. Kwa hiyo huo ndio Ushahidi wa nia yake ya dhati ninayoweza kuelezea.”
Hata hivyo Breyer anapanga kubaki katika mahakama mpaka mwisho wa muhula wake mwezi Juni au hadi pale nafasi yake itakapojazwa na Biden na kuthibitishwa na Baraza la Seneti.