Hatua hiyo itaanza Januari 30 kwa shirika la ndege la Xiamen Airlines linalofanya safari zake kutoka Los Angeles kwenda Xiamen hadi Machi 29, Wizara ya Usafirishaji imesema.
Uamuzi huo utasitisha baadhi ya safari za ndege za Xiamen, Air China, China Southern Airlines na China Eastern Airlines.
Tangu Disemba 31, mamlaka nchini China zimesitisha safari za ndege 20 za United Airlines, 10 za shirika la ndege la American Airlines na 14 za Delta Airlines, baada ya baadhi ya wasafiri kugundulika walikuwa na maambukizi ya COVID-19.
Jumanne, Wizara ya Usafirishaji imesema serikali ya China ilikuwa imetangaza kufuta kwa safari mpya za ndege za Marekani.
Liu Pengyu, msemaji wa Ubalozi wa China Washington, alisema Ijumaa sera ya safari za ndege za abiria za kimataifa zinazoingia China “zimetumika sawa na zile zilizotumika kwa mashirika ya ndege ya China na ya kigeni kwa njia ya haki, na uwazi.”
Ameiita hatu ya Marekani “haikuwa ya busara” na kuongeza, “Tunausihi upande wa Marekani kuacha kuvuruga na kuweka masharti kwa safari za kawaida za ndege za abiria” za mashirika ya ndege ya China.
Airlines for America, kikundi cha biashara kinachowakilisha mashirika ya ndege matatu ya Marekani yaliyoathiriwa na hatua ya China, yakiwemo mengine, wamesema wanaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Marekani “ili kuhakikisha uadilifu jinsi yanavyotendewa mashirika ya ndege ya Marekani katika soko la China.”
Wizara ya Usafirishaji imesema Ufaransa na Ujerumani wamechukua hatua kama hizo dhidi ya hatua za kudhibiti COVID-19 zilizochukuliwa na China. Imesema hatua ya China kusitisha safari za ndege “ zinakiuka maslahi ya umma na zinahalalisha hatua zinazowiana katika kutatua hilo.
Imeongeza kuwa kitendo cha hatua ya peke yake iliyochukuliwa na China dhidi ya mashirika ya ndege yaliyotajwa ya Marekani haiendi sambamba na mikataba ya ushirikiano wa pande mbili.
China pia imesitisha safari za mashirika ya ndege ya China mbalimbali yanayokuja Marekani baada ya abiria baadae kugundulika wana maambukizi.
Wizara hiyo imesema iko tayari kupitia tena hatua zake kama China itaangalia tena “sera zake ili kufanya marekebisho muhimu katika hali hii kwa mashirika ya ndege ya Marekani.”
End