Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 26, 2024 Local time: 21:07

India: Modi kulazimika kushirikisha upinzani serikalini kufuatia uchaguzi mkuu


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akionyesha ishara ya ushindi.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akionyesha ishara ya ushindi.

Muungano wa kisiasa unaoongozwa na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, umeshinda viti vichache kwenye bunge, lakini changamoto kubwa kutoka kwa upinzani, imepunguza kwa kiasi kikubwa, ukubwa wa chama chake, na kuashiria kupungua kwa umaarufu wake baada ya muongo mmoja madarakani.

Chama cha Modi cha Hindu Bharatiya Janata Party (BJP), pamoja na washirika wake, kilipata viti 294 kati ya 543, vilivyokuwa vikishindaniwa katika baraza la chini la bunge.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, Modi alisema kwamba "watu wameweka imani yao katika NDA, kwa mara ya tatu mfululizo, na kwamba hilo sijambo la kawaida katika historia ya India.

Aliwahakikishia wananchi kwamba atandeleza kazi nzuri iliyofanywa katika mwongo mmoja uliopita ili kuendelea kutimiza matarajio yao. NDA ni Muungano wa Kitaifa wa Kidemokrasia unaoongozwa na BJP.

Lakini, katika kile kinachoonekana kama kupungua kwa umaarufu kwa kiasi kikubwa, kwa kiongozi huyo wa India, ambaye ametawala nchi hiyo akiwa na umaarufu mkubwa katika muongo mmoja uliopita, BJP haikuweza kupata wingi wa wazi wa kura, ikiwa peke yake.

Chama kilishinda viti 240 - pungufu ya viti 272 vinavyohitajika kwa wingi wa kura zilizohesabiwa hadi Jumanne jioni. Hiyo ni idadi ndogo, iklinganishwa na viti 303 ambavyo kilishinda katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2019.

Forum

XS
SM
MD
LG