Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 08, 2025 Local time: 09:40

Viongozi wa Afrika watia saini takriban mikataba 50 na Korea Kusini


Mkutano wa viongozi wa nchi na serikali za Afrika na Korea Kusini.
Mkutano wa viongozi wa nchi na serikali za Afrika na Korea Kusini.

Takriban makubaliano na mikataba 50 imetiwa saini wakati wa mkutano wa kwanza wa kilele wa Korea Kusini na viongozi kutoka nchi 48 za Afrika, ili kushirikiana katika masuala yanayohusu  madini, nishati na utengenezaji wa bidhaa, wizara ya viwanda ya Korea Kusini ilisema Jumatano.

Kampuni ya Korea Kusini ya Hyosung Corp ilitia saini mkataba wa kusambaza transfoma za umeme nchini Msumbiji zenye thamani ya dola milioni 30, wizara ilisema katika taarifa.

Wizara ya viwanda pia ilitia saini makubaliano ya kushirikiana katika madini muhimu na Madagaska na Tanzania, ili kupata vifaa kwa ajili ya viwanda kama vile betri, ilisema taarifa hiyo.

Makubaliano hayo 47 na mataifa 23 ya Afrika yalifanywa wakati wa mkutano huo huku nchi hiyo ya nne kwa ukubwa wa kiuchumi barani Asia, ikinuia kupata soko kubwa la nje, barani Afrika.

"Pamoja na uwezo wake mkubwa, Afrika bado inachangia asilimia 1-2 tu ya biashara na uwekezaji wa Korea Kusini..." Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol aliuambia mkutano huo wa kibiashara, wa viongozi 200 wa kisiasa na viwanda kutoka nchi za Afrika na Korea Kusini, siku ya Jumatano.

"Matumaini yangu ni kwamba ushirikiano wa rasilimali wenye manufaa kwa pande zote utapanuliwa," Yoon alisema.

Yoon aliahidi Jumanne kwamba Korea Kusini itaongeza msaada wa maendeleo kwa Afrika hadi dola bilioni 10 katika kipindi cha miaka sita ijayo, na kusema itatoa dola bilioni 14 katika ufadhili wa mauzo ya nje ili kukuza biashara na uwekezaji kwa makampuni ya Korea Kusini barani Afrika.

Viongozi wa nchi za Afrika na Korea Kusini kuimarisha ushirikiano kati yao
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:17 0:00

Forum

XS
SM
MD
LG