Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 18:52

Hatma ya Spika McCarthy kujulikana leo, akabiliwa na upinzani nadra wa Mrepublikan mwenzake


Speaker of the House Kevin McCarthy, talks to reporters after a closed-door meeting with House Republicans after Rep. Matt Gaetz filed a motion to oust McCarthy from his leadership role, at the Capitol in Washington, Oct. 3, 2023.
Speaker of the House Kevin McCarthy, talks to reporters after a closed-door meeting with House Republicans after Rep. Matt Gaetz filed a motion to oust McCarthy from his leadership role, at the Capitol in Washington, Oct. 3, 2023.

Wabunge wa Marekani wataamua Jumanne iwapo Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy ataendelea na uongozi wake baada ya kukabiliwa na upinzani nadra kutoka kwa mwanachama wa chama chake.

Mwakilishi Mrepublikan Matt Gaetz aliwasilisha hoja Jumatatu jioni kulazimisha ipigwe kura ya kumuondoa McCarthy, akisema amechoshwa na uongozi wa McCarthy baada ya McCarthy kushindwa kupitisha mswaada wa ufadhili wa serikali wiki iliyopita kwa kuzingatia vipaumbele vya matumizi ya Waconservative.

Matt Gaetz
Matt Gaetz

Hakuna spika wa Baraza la Wawakilishi ambaye aliyewahi kuondolewa katika nafasi yake.

“Kama ningehesabu ni mara ngapi watu wametaka kuniondoa katika nafasi yangu, ningekuwa tayari nimeshaondoka siku nyingi,” McCarthy aliwaambia waandishi wa habari Jumanne asubuhi.

Kura ya kumuondoa McCarthy itahitaji wingi mdogo katika Baraza la Wawakilishi lenye wajumbe 435. Warepublikan wanadhibiti baraza hilo kwa idadi ya wajumbe 221 dhidi ya 212 wapinzani wa Wademokratik.

Ikitegemea ni wawakilishi wangapi wanahudhuria kikao na upigaji kura katika ukumbi wa Bunge, McCarthy anaweza kumudu kubaki katika nafasi yake kama ni wabunge Warepublikan sita hawatampigia kura.

Ni ripoti ya mwandishi wa VOA, Katherine Gypson.

Forum

XS
SM
MD
LG