Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:27

Guinea: Watu kadhaa wafariki kutokana na ajali ya moto Conakry, juhudi zaendelea kuuzima


Moto ukiendelea kuwaka katika kituo cha mafuta.
Moto ukiendelea kuwaka katika kituo cha mafuta.

Mlipuko na moto katika ghala kuu ya mafuta nchini Guinea kwenye mji mkuu Conakry umesababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine , mamlaka na vyombo vya habari vimeripoti Jumatatu, wakati huduma za dharura zikipambana kuuzima moto huo.

Moto ulilipuka katika kiwanda cha mafuta ya petrol muda mfupi baada ya mlipuko mkubwa kutokea usiku wa jumapili , ofisi ya rais wa Guinea imesema katika taarifa yake.

Eneo hilo lililoko katika wilaya ya Kaloum ina maofisi mengi ya serikali.

Haikuelezwa wazi nini kimesababisha moto huo katika kiwanda ambapo kinasambaza mafuta kwenye maeneo mengi ya Guinea, hali iliyozusha hofu ya kuvurugika kwa usambazaji mkubwa.

Maafisa hawajathibitisha idadi ya majeruhi ingawa vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa maelfu ya watu wamejeruhiwa wengi wao wamelazwa hospitali wakiwa na majeraha mabaya.

Takriban watu wanne wamethibitishwa kuwa wamekufa katika hospitali ya Iganace Deen, shirika la habari lenye makao yake Conakry , Le carrier de Conakry limeripoti.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG