Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:19

Moto kwenye kituo kikuu cha mafuta wajeruhi watu kadhaa mjini Conakry, Guinea


Moto uliyozuka kwenye kituo kikuu cha mafuta mjini Conakry.
Moto uliyozuka kwenye kituo kikuu cha mafuta mjini Conakry.

Serikali ya Guinea imeamuru shule kufungwa pamoja na wafanyakazi kubaki nyumbani Jumatatu kwenye mji mkuu wa Conakry kufuatia moto mkubwa uliyotokea kwenye kituo kikuu cha kuhifadhia mafuta na kusababisha  kujeruhiwa kwa watu kadhaa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, moto huo uliyoandamana na mlipuko ulisababisha wingu kubwa la moshi mweusi angani, wakati wakazi wa karibu na eneo hilo wakikimbilia usalama wao, kulingana na video na picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Moto huo ulizuka muda mfupi baada ya saa sita za usiku karibu na bandari kulingana na vyombo vya habari vya ndani pamoja na wakazi waliozungumza na AFP. Chanzo cha moto huo hakijabainishwa, ingawa maafisa wamesema kwamba huenda ukawa na athari kwa watu wa taifa hilo.

Daktari mmoja wa upasuaji kwa jina Mamadouba Sylla kutoka hospitali ya Donka mjini Conackry ameambia AFP kwamba darzeni ya watu walijeruhiwa, wengi wao wakipelekwa kwenye hospitali za Donka na Ignace Deen. Serikali imesema kwamba vituo vya mafuta vitabaki kufungwa kwa saa kadhaa, wakati uchunguzi ukianzishwa ili kubaini chanzo cha moto huo.

Forum

XS
SM
MD
LG