Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:09

Kiongozi wa zamani kijeshi wa Guinea atolewa jela na watu wenye silaha


Kiongozi wa zamani wa kijeshi Moussa Dadis Camara.
Kiongozi wa zamani wa kijeshi Moussa Dadis Camara.

Aliyekuwa kiongozi wa kundi la kijeshi lililofanya mapinduzi ya Guinea 2008 Moussa Dadis Camara, Jumamosi leo ametolewa jela na kundi la wanaume waliokuwa wamejihami mjini Conakry.

Camara amefunguliwa akiwa na maafisa wengine watatu wa ngazi ya juu, kulingana na waziri wa Sheria Charles Wright. Wakazi wa Conakry wameambia shirika la habari la Reuters kwamba magari ya kijeshi pamoja na vikosi maalum vilikiuwa vikishika doria baada ya milio ya risasi kusikika kwenye eneo la kiutawala la Kaloum, ambako Camara na wenzake walikuwa wameshikiliwa kwenye jela ya Central House.

Waziri Wright wakati akitoa taarifa hizo kwa njia ya radio amesema kwamba wanasakwa na kwamba watapatikana popote walipo, bila kutoa maelezo zaidi. Ameongeza kusema kwamba mipaka ya Guinea imefungwa ili kuzuia Camara na wenzake kutoroka nchini.

Kiongozi huyo na wenzake wamekuwa mahakamani tangu mwaka jana wakituhumiwa kuchochea mauaji kwenye uwanja wa michezo, ambako pia wanawake walibakwa na vikosi vya usalama vya Guinea, na kupelekea vifo vya watu 150, wakati wa mkutano wa kuitisha demokrasia Septemba 28, 2009.

Camara hata hivyo amekanusha mashitaka hayo, wakati akilaumu wanajeshi waasi. Guinea inatawaliwa na kiongozi wa kijeshi Mamady Doumbouya ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya 2021 ambayo ni ya 8 kufanyika Afrika Magharibi na Kati ndani ya miaka mitatu iliyopita. Mali, Niger, Burkina Faso na Gabon zinaongozwa na utawala wa kijeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG