Miili mitano ilipatikana chini ya vifusi siku ya Jumanne baada ya majengo mawili kuanguka siku ya Jumatatu huko Conakry, katika mji mkuu wa Guinea, serikali imesema.
Majengo hayo yalianguka majira ya saa kumi na moja kwa saa za huko, katika kitongoji cha kusini cha Matoto, msemaji wa serikali alisema katika taarifa ya Jumanne.
Serikali inatoa pole kwa familia na wapendwa wa waathirika na inawaombea kupata nafuu ya haraka majeruhi, ilisema taarifa hiyo. Waziri wa sheria aliamuru ufanyike uchunguzi wa mahakama, ilisema taarifa.
Timu za uokoaji zilipata miili minne ndani ya saa 24 baada ya ajali hiyo, Togba Isaac Kolie, mkuu wa idara ya ulinzi wa raia, aliliambia shirika la habari la AFP mapema Jumanne. Ajali hiyo ilitokea wakati timu ya ujenzi ilipoanza kuongeza ghorofa ya sita kwenye jengo hilo, mfanyakazi mmoja wa ujenzi alisema.
Forum