Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:57

Ghasia zaripotiwa kati ya makundi hasimu yenye silaha ya Libya


Picha ya maktaba ya wanajeshi wa Libya
Picha ya maktaba ya wanajeshi wa Libya

Ghasia kati ya makundi mawili ya wanamgambo kwenye mji mkuu wa Libya, yamehangaisha wakazi na kuuwa takriban watu darzeni moja, zikiwa za karibu zaidi kwenye taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika, lisilo na sheria, maafisa wamesema.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, makabiliano hayo yametokea Ijumaa kwenye kitongoji cha mashariki mwa mji wa Tripoli, cha Tajoura, yakihusisha kundi la Rahba al Duruae linaloongozwa na Bashir Khaifallah dhidi ya lile la al Shadida Sabriya, taarifa zimeongeza.

Huduma za dharura za wizara ya afya zimesema kwamba takriban watu 9 waliuwawa na wengine 16 kujeruhiwa kwenye ghasia hizo zilizochukua saa kadhaa. Ghasia hizo zilisababishwa na jaribio la mauaji dhidi ya al Baqrah Ijumaa, ambalo kundi lake lililaumu lile la al Shahida Sabriya, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Makundi yote mawili yanahusishwa na serikali ya waziri mkuu Abdul Hamid Dbeibah, na msemaji wake hakusema lolote kuhusiana na tukio hilo. Ghasia hizo zinaashiria kuyumba yumba kwa taifa hilo lililokumbwa na vita tangu mapinduzi ya 2011, yaliomuondoa dikteta wa muda mrefu Moammar Gadhafi.

Forum

XS
SM
MD
LG