Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:17

Watu 12 wahukumiwa Libya kwa kubomoka kwa bwawa la maji


Mahakama ya Libya, Jumapili imewahukumu maafisa 12 wa sasa na zamani kifungo cha hadi miaka 27 gerezani kwa kuhusika kwao katika kubomoka kwa mabwawa mawili mwaka jana.

Tukio hilo lilisbabisha maji kwenda juu katika ukuta kwa mita kadhaa katikati ya mji wa pwani. Maelfu ya watu walipoteza maisha kutokana na tukio hilo.

Mabwawa hayo mawili nje ya mji wa Derna yalivunjika Septemba 11 baada ya kuzidiwa na kimbunga Daniel, ambacho kilisababisha mvua kubwa mashariki mwa Libya. Kushindwa kwa miundombinu yake kulisababisha kumezwa kwa robo ya jiji, kuharibu vitongoji vyote na kusukuma watu baharini maafisa wamesema.

Mahakama ya jinai ya Derna, Jumapili iliwakuta na hatia maafisa 12 wa sasa na wa zamani kwa usimamizi mbovu, uzembe na makosa ambayo yalichangia maafa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa nchi.

Washitakiwa hao waliokuwa na jukumu la kusimamia mabwawa ya maji nchini, walipewa vifungo vya kati ya miaka 9 hadi 27, imesema taarifa bila kuwataja. Washtakiwa watatu kati ya hao waliamriwa kurejesha fedha zilizopatikana kwa njia haramu, imesema taarifa bila kufafanua. Mahakama imewaachia huru watu wengine wanne.

Hukumu ya Jumapili inaweza kukatiwa rufaa mbele ya mahakama ya juu, kutokana na mfumo wa mahakama wa Libya.

Taifa hilo la Afrika Kaskazini lenye utajiri mkubwa wa mafuta limekuwa katika machafuko toka 2011 wakati uasi ulioungwa mkono na NATO na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomng’oa madarakani kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi, ambaye aliuwawa baadaye.

Kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, tawala hasimu zimedai mamlaka ya kuongoza Libya.

Kila moja inaungwa mkono na makundi yenye silaha na serikali za kigeni.

Forum

XS
SM
MD
LG