Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:30

Fayulu apinga matokeo yaliyompa ushindi Tshisekedi


Martin Fayulu
Martin Fayulu

Mgombea aliye chukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anapinga matokeo rasmi yanayo onyesha kuwa Tshisekedi ni mshindi katika kura iliyopigwa Disemba 30 kuwa siyo ya kweli.

Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, CENI, imetangaza mapema Alhamisi kuwa Tshisekedi ameshinda kwa zaidi ya kura asilimia 38, kitu kilicho washangaza wasimamizi wa uchaguzi baada ya kura za maoni kabla ya uchaguzi kuelekeza kuwa kiongozi mwanzake wa upinzani Martin Fayulu atashinda uchaguzi huo.

Fayulu, ambaye ameshinda kura asilimia 34, ametuhumu tume hiyo kwa kufanya “mapinduzi ya uchaguzi,” na kuwataka Kanisa Katoliki kutoa matokeo ya majumuisho ya hesabu za kura zinazo jitegemea.

Baadhi ya wanadiplomasia wameviambia vyombo vya habari kuwa kura zilizo kuwa zimehisabiwa na timu ya waangalizi wa Kanisa zinaonyesha Fayulu ni mshindi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian pia alieleza kutilia mashaka matokeo hayo, akikiambia kituo cha habari cha Ufaransa CNews Alhamisi kuwa matokeo rasmi yanapingana na hesabu halisia.

Matokeo rasmi yanaweza kuchochea dhana ya kuwa Rais anayeondoka madarakani Joseph Kabila alifanya makubaliano na Tshisekedi kwamba amtangaze kuwa mshindi.

Emmanuel Ramazani Shadary, mrithi aliyekuwa amechaguliwa na Rais Kabila alichukuwa nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro hicho.

Iwapo matokeo yatabakia kama yalivyo, itawezesha nchi hiyo kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia kwa mara ya kwanza tangu ipate uhuru kutoka Ubelgiji mwaka 1960.

XS
SM
MD
LG