Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:02

EU yasitisha kwa muda ufadhili wa mpango wa chakula kwa Somalia 'kutokana na wizi'


Mpngo wa Umoja wa Mataifa wa Chakula Duniani WFP.
Mpngo wa Umoja wa Mataifa wa Chakula Duniani WFP.

Umoja wa Ulaya umesitisha kwa muda ufadhili wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Somalia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wizi na utumiaji mbaya wa misaada.

Hayo ni kwa mujibu wa maafisa wawili wakuu wa Umoja huo waliozungumza ma shirika la habari la Reuters siku ya Jumatatu, baada ya uchunguzi kubaini" wizi mkubwa na matumizi mabaya ya misaada," ambayo ilikuwa na lengo la kuepusha baa la njaa.

Tume ya Ulaya ilitoa msaada wa zaidi ya dola milioni 7 kwa operesheni za WFP nchini Somalia mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya zaidi ya dola bilioni moja ilizopokea katika michango yote, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Nchi wanachama wa EU zilitoa pesa nyingi zaidi, kwa misingi ya ushirikiano wa nchi kwa nchi.

Haikubainika mara moja ikiwa kuna nchi yoyote binafsi ambayo pia angesitisha msaada. Balazs Ujvari, msemaji wa Tume ya Ulaya, hakuthibitisha wala kukanusha moja kwa moja taarifa za kusimamishwa kwa misaada kwa muda lakini alisema: "Hadi sasa, EU haijafahamishwa na washirika wake wa Umoja wa Mataifa kuhusu athari za kifedha kwa miradi inayofadhiliwa na muungano huo.

WFP haikujibu mara moja ombi la shirika la habari la Reuters, la kutaka itoe kauli kuhusu suala hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG