Kiongozi mashuhuri wa upinzani Misri Mohamed ElBaradei amewambia maelfu ya waandamanaji kati kati ya Cairo kwamba "hatuwezi kurudi nyuma" baada ya kuanza upinzani wa umaa dhidi ya Rais Hosni Mubarak wa Misri.
Waandamanaji wanakaidi amri ya serikali ya kutotoka nje usiku kwa siku ya tatu mfululizo wakiendelea na madai yao ya kumtaka Bw Mubarak kuondoka baada ya zaid ya miaka 30 madarakani.
Ndege za kijeshi ziliruka juu ya uwanja mkuu wa Cairo wa Tahrir, kituo kikuu cha upinzani dhidi ya rais, mchana wa Jumapili wakati waandamanaji walikua waliwasalia zaidi ya waandamanaji 100 walouwawa wakati wa maandamano tangu Jumanne.
ElBaradei, mkuu wa zamani wa Idara ya nuklia ya Umoja wa Mataifa, aliviambia vituo vya televisheni vya CNN na CBS, kwamba ana madaraka aliyopewa na wananchi wa Misri na upinzani kukubaliana juu ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Vile vile amesema kwamba sera za Marekani kuelekea Misri imeanza "kutoaminika" kwa kutoa wito wa mabadiliko ya kidemokrasia na huku ikielndelea kumunga mkono rais wa Misri. Amesema ni lazima kwa Bw Mubarak kuondoka Misri "leo"