Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 20:35

Maandamano zaidi Mashariki ya Kati


Wayemen wanaoipinga serikali wanandamana kumtaka rais Ali Saleh kuondoka madarakani.
Wayemen wanaoipinga serikali wanandamana kumtaka rais Ali Saleh kuondoka madarakani.

Siku moja baada ya mapinduzi ya wananchi wa Misri maelfu ya wandamanaji walikjusanyika katika mji mkuu wa Yemen Sanaa JUmamosi kumtaka Rais Ali Abdullah Saleh kuondoka nmadarakani baada ya miongo mitatu madarakani.

Huko Algiers waandamanaji elfu mbili walikaidi marufuku iliyotolewa na serikali na walikumbana na polisi elfu 30 walowakamata mamia ya watayarishaji wa maandamano hao.

Maandamano ya Yamen yalianza kwa waandamanaji kuelekea kwenye ubalozi wa Misri lakini kabla ya kuwasili walipambana na waandamanaji wanaoiunga mkono serikali. Waandamanaji wanaoipinga serikali walionekana wakiwa na lengo la kufika hadi chuo kikuu cha Sana'a na kuigeuza kuwa sawa na uwanja wa tahrir kitovu cha mapinduzi ya Misri.

Sawa na Bw Mubarak, Rais Ali Saleh amekua madarakani tangu 1978, na katika juhudi za kupunguza malalamiko ameahidi kwamba hatogombania mhula mwengine baada ya mhula wake kumalizika 2013.

Wakati huo huo huko Algiers polisi walipambana na waandamanaji na serikali imetangaza kwamba itaondoka karibuni hali ya dharura iliyotangzawa miaka 19 baada ya kuzuka uwasi wa wanaharakati wa kislamu nchini humo.

XS
SM
MD
LG