Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 22:47

Serikali mpya ya Tunisia ipo mashakani


Polisi wa kutuliza ghasia akikutana uso kwa uso na waandamanaji katika mji mkuu Tunis, Tunisia, 18 Jan 2011
Polisi wa kutuliza ghasia akikutana uso kwa uso na waandamanaji katika mji mkuu Tunis, Tunisia, 18 Jan 2011

Hali ya baadaye ya serikali ya muda nchini Tunisia ilikuwa mashakani Jumanne kufuatia kujiuzulu kwa mawaziri wasiopungua wanne na maandamano mapya kujitokeza tena.

Chini ya saa 24 baada ya Waziri Mkuu wa Tunisia, Mohammed Ghannouchi, kutangaza serikali mpya, mamia ya waandamanaji walirudi mitaani wakiimba nyimbo kupinga hatua hiyo.
Kama ilivyokuwa siku za nyuma, polisi wa kutuliza ghasia walivunja maandamano kwa kutumia gesi ya kutoa machozi na waliwasaka waandamanaji.


Maandamano hayo yamekuja kufuatia mawaziri wanne wa serikali ya muda kujiuzulu. Mawaziri watatu walikuwa wanachama wa chama cha wafanyakazi cha UGTT, ambacho kilihusika kikamilifu katika maandamano ya kitaifa wiki iliyopita, ambayo yalipelekea kuondolewa madarakani kwa Rais wa muda mrefu nchini humo Zine el-Abidine Ben Ali. Wanachama wa muungano huo walisema hawakuweza kubaki katika serikali dhalimu iliyoongozwa na chama tawala cha RCD cha Ben Ali, ambacho kililalamikiwa vikali kuwa na rushwa na unyanyasaji.

Wakati wa mkutano na waandishi habari, Ghannouchi alisema kipaumbele cha serikali ya mpito ni kurudisha usalama baada ya siku kadhaa ya wizi wa ngawira na mandamano, lakini aliahidi mageuzi ya kisiasa na kiuchumi. Kaimu Rais Fouad Mebazaa ametangaza kwamba uchaguzi utafanyika katika muda wa siku 60 zinazokuja.

Lakini nafasi zote za juu katika wizara ya ulinzi, fedha, mambo ya ndani na nje zimebaki mikononi mwa serikali ya zamani ya Rais aliyepinduliwa Zine el-Abidine Ben Ai. Serikali hiyo mpya haikuwahusisha wajumbe wa vyama kadha vya upinzani vya mrengo wa kushoto na ki-Islamu, vilivyokua vimepigwa marufuku chini ya utawala wa Ben Ali.

Hata kabla ya serikali hiyo mpya kutangazwa mamia ya waandamanaji kwa mara nyingine tena walikusanyika katika barabara kuu ya Tunis ya Habib Bourgiba wakimbia kuondolewa kwa chama tawala cha Ben Ali cha RCD.

XS
SM
MD
LG