Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 29, 2024 Local time: 00:31

Rais wa Tunisia akimbia nchi


Watunisia wakiandamana kumtaka rais Ben Ali kuacha madaraka Januari 14, 2011
Watunisia wakiandamana kumtaka rais Ben Ali kuacha madaraka Januari 14, 2011

Rais wa muda mrefu wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali, amelazimika kukimbia nchi siku ya Ijumaa, kufuatia kishinikizo kikubwa cha wananchi na ghasia za wiki kadhaa kumtaka kuacha madaraka. Waziri mkuu Mohamed Ghannouchi ametangaza kwamba amechukua madaraka ya muda ya nchi hiyo.

Ben Ali aliyetawala kwa miaka 23 aliondoka kwa ndege maalum Ijumaa usiku na haikujulikani anaelekea wapi. Jeshi lilifunga uwanja wa ndege na mipaka ya anga kwa muda.

Baadhi za ripoti zilieleza kwamba huwenda Bw Ben Ali alisafiri kuelekea Malta lakini waziri wa mambo ya nchni za nje wa Tunisia anaripotiwa kukanusha habari hizo.

Taifa la kikoloni la zamani la Tunisia, Ufraransa linaripotiwa kueleza kwamba Bw Ben Ali alitaka kuonana na rais Nicolas Sarkozy ambae amekata kumpokea. Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ufaransa inakanusha pia habari kwamba kiongozi huyo ameomba hifadhi ya kisiasa, ikieleza kwamba itashauriana kwanza na utawala mpya wa Tunisia.

Kabla ya kuondoka Tunis, Bw Ben Ali aliivunja serikali na kutangaza hali ya dharura nchini humo. Na ripoti zinaeleza kwamba waandamanaji wamekaidi amri hiyo na wamefika mbele ya ikulu na kumtaka waziri mkuu kuondoka na kumkabidhi mamlaka spika wa bunge.

Jumuia ya kimataifa inafuatilia kwa makini matokeo hayo ya Tunisia.

XS
SM
MD
LG