Polisi huko Tunisia wamewaweka washirika wakuu wawili wa rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali kwenye kifungo cha nyumbani, na kumkamata mmiliki wa kituo kimoja binafsi ambae anauhusiano na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani.
Vyombo vya habari vya serikali viliripoti Jumapili kwamba, Larbi Nasra, mmiliki wa Hannibal TV, na jama yake mke wa rais wa zamani Ben Ali, alikamatwa kwa madai ya uhaini.
Watu wengine waliokamatwa walikuwa msemaji wa rais wa zamani Abdelaziz Ben Dhia na mkuu wa baraza la Seneti Abdallah Kallel.
Wakati huo huo wanadamanaji waliendelea kudai kuondolewa kila mtu aliyehusika au kushiriki katika utawala wa rais wa zamani aliyekimbia nchi mapema mwezi huu. Mamia ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Tunis Jumapili hadi wakati wa usiku wakidai kwamba mawaziri na maafisa wote walokua katika utawala wa Ben Ali wasihusishwe na serikali mpya.
wandamanaji walikusanyika usiku mzima mbele ya afisi ya waziri mkuu kumtaka kaimu rais na waziri mkuu walokuwa katika serikali iliyoondoelwa, waondoke madarakani.