Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 09, 2025 Local time: 10:36

Obama: Lazima mpito ufanyike kwa amani na sasa hivi Misri


Rais Hosni Mubarak wa Misri akilihutubia taifa Ferbuari 1 2011 akisema hatogombania tena madaraka.
Rais Hosni Mubarak wa Misri akilihutubia taifa Ferbuari 1 2011 akisema hatogombania tena madaraka.

Rais Barack Obama wa Marekani anasema amemuambia kiongozi mwenzake anaekabiliwa na uwasi wa wananchi kwamba, "kipindi cha mipto ni lazima kifanyike kwa amani na kuanza mara moja".

Katika ujumbe wake kupitia telivisheni Jumanne usiku, Rais Obama alisema ni lazima kwa kipndi cha mpito kipeleke kufanyika uchaguzi wa huru na haki huko Misri na matokeo ni kuundwa serikali ya kidemokrasia itakayo jibu matakwa ya wananchi wa Misri.

Rais wa Marekani alizungumza na Bw. Mubarak baada ya kiongozi huyo kuwahutubia wananchi wake na kuwambia kwamba hatogombania tena mhula mwengine.

Katika hotuba yake Bw. Mubarak amesema ametumia maisha yake yote kuitumikia Misri na wananchi wake. Alisema hatoihama nchi na atakufa nchini humo, badala yake anasema atafanya kazi katika miezi iliyobaki ya mhula wake kuhakikisha kuna mageuzi yanayofanyika na kukabidhi madaraka kwa amani.

George Kakoti, mhadhiri wa chuo kikuu cha Florida ameiambia Sauti ya Amerika-VOA, kwamba Rais Obama amejaribu kuonesha kwamba yeye siye ndiye analazimisha mageuzi yeyote, na wakati huo huo anataka kuiweka Marekani katika mahala ambapo, matokeo yeyote yale hayata athiri uhusiano wake na Misri.

XS
SM
MD
LG