Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:43

China yajizatiti 'kuongoza' katika teknolojia muhimu za kijeshi


FILE - Magari ya kijeshi yaliyobeba makombora ya hypersonic, Beijing, China Oct. 1, 2019.
FILE - Magari ya kijeshi yaliyobeba makombora ya hypersonic, Beijing, China Oct. 1, 2019.

Utafiti wa China katika baadhi ya teknolojia muhimu za kijeshi imepiga hatua kiasi cha kwamba Marekani na washirika wake wakuu inawezekana wasiweze kuwafikia, kulingana na uchambuzi mpya uliofanywa na Taasisi ya Utafiti ya Australia.

Taasisi ya Sera za Usalama ya Australia (ASPI) ilitoa matokeo yake Jumanne yaliyojikita katika tathmini ya asilimia 10 ya utafiti bora wa hali ya juu zaidi, zikihitimisha kuwa China inaongoza katika fani 19 kati ya 23, ikiwemo baadhi ambazo zinaweza kuifanya iwe na jukumu kubwa katika jitihada ya Beijing kupata umashuhuri wa kijeshi katika kanda ya Indo-Pacific na kwengine.

China “inaongoza katika ndege zinazokwenda kwa kasi kubwa, vifaa vya kivita vya kielektroniki na katika uwezo wake wa shughuli za chini ya bahari,” utafiti wa ASPI uligundua, ukitahadharisha kuwa, “China inaongoza kwa hali ya juu sana na wanasababisha hatari kubwa kwamba China inaweza kuchukua nafasi ya juu siku za usoni katika uvumbuzi wa kiteknolojia katika maeneo haya.”

Uchambuzi huu umegundua zaidi kuwa kwa ndege zinazokwenda kwa kasi, tisa kati ya taasisi za utafiti 10 zinazoongoza ziko China, wakati China ni nyumbani kwa vituo vya utafiiti 10 vya juu kwa droni za chini ya bahari.

Kinyume cha makombora ya masafa marefu, ambayo yanasafiri kwa spidi kubwa zaidi lakini kwa njia iliyopangiwa, silaha za kusafiri kwa kasi zinaweza kurekebishwa licha ya kuruka kwa spidi mara tano inavyosafiri sauti.

Na mwanya kati ya China na nchi nyingine ni mkubwa. Huku baadhi ya teknolojia hizo, kama vile silaha na ndege zinazokwenda kwa kasi, China inatoa zaidi ya asilimia 73 ya utafiti wenye umuhimu mkubwa, kuliko Marekani na nchi nyingine nane zinazofuatwa zikijumuishwa pamoja.

Uchambuzi huo pia umegundua kunaviashiria kwamba China inatumia taasisi za utafiti za nchi za Magharibi kwa maslahi yake.

Forum

XS
SM
MD
LG