Waziri wa ulinzi wa China siku ya Jumapili alitetea kupita kwa meli ya kivita mbele ya meli ya kivita ya Marekani na meli ya Canada wakati zikisafiri kupitia mlango bahari wa Taiwan, akidai kwamba kupita kwa meli za mataifa ya magharibi kwa madaia ya kupiga doria katika bahari huru nio uchokozi kwa China.
Marekani na Canada zilifanya safari hiyo nadra ya pamoja kupitia mlango wa bahari wa Taiwan siku ya Jumamosi, huku meli ya kivita ya China ikiipita meli ya Marekani na kugeuza upinde wake kutoka mita 140 (yadi 131) kwa njia isiyo salama, kulingana na makao makuu ya kijeshi ya Marekani katika kanda ya Indo-Pacific.
Mchambuzi wa siasa za kimataifa David Monda anaelezea kwa kina suala hili.
Forum