Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:30

Meli za kivita za China zimezingira Taiwan


Ndege na meli za kivita za China
Ndege na meli za kivita za China

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema kwamba imegundua meli tatu za kivita za China, ikiwemo meli ya Shandong, inayobeba ndege za kivita, zikipita kwenye mlango wa bahari wa Taiwan.

Tukio hilo limejiri wakati China inaendelea kusisitiza kwamba kisiwa cha Taiwan, kinachojitawala, ni sehem ya himaya yake.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema kwamba inaendelea kufuatilia mienendo ya meli hizo na itajibu inavyostahiki.

Katika ujumbe wa Twitter, wizara hiyo imesema kwamba meli hizo tatu zilikuwa zinaelekea kaskazini mwa bahari ya Taiwan, na zimepita sehemu ya mpaka wa bahari usio rasmi ambao kila upande uliwahi kudai kuwa sehemu yake.

China imeongeza harakati zake za kijeshi karibu na Taiwan katika miezi ya hivi karibuni, huku uhusiano kati ya China na Marekani ukiendelea kuwa mbaya.

China imedai kwamba Taiwan ni sehemu yake na kwamba inadhibiti uongozi wa kisiwa hicho kwa nguvu iwapo litahitajika kufanya hivyo.

Taiwan imesema kwamba ndege za kivita na meli 10 za jeshi la China zimeonekana kuzunguka Taiwan katika muda wa saa 24 zilizopita.

Forum

XS
SM
MD
LG