Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:56

Jeshi la Marekani lasema ndege ya kivita ya China yaruka karibu na ndege yake ya upelelezi

Pichani kutoka kwenye video iliyotolewa na Jeshi la Wanamaji la Marekani, ndege ya kivita ya China J-16 ikiruka kwa fujo karibu na ndege ya Marekani RC-135 inayoruka katika anga ya kimataifa juu ya Bahari ya Kusini ya China siku ya Ijumaa, Mei 26, 2023.

Jeshi la Marekani linasema kuwa ndege ya kivita ya China iliruka karibu na mojawapo ya ndege zake za upelelezi wakati wa operesheni ya doria katika Bahari ya South China wiki iliyopita.

Jeshi la Marekani linasema kuwa ndege ya kivita ya China iliruka karibu na mojawapo ya ndege zake za upelelezi wakati wa operesheni ya doria katika Bahari ya South China wiki iliyopita.

Taarifa ya Kamandi ya Marekani ya Indo-Pacific inasema ndege ya kivita ya China J-16 iliruka moja kwa moja mbele ya ndege ya RC-135 katika uendeshaji wa fujo usio wa lazima na kumlazimu rubani kuruka katikati ya machafuko yaliyosababishwa na ndege hiyo ya kivita.

Picha za video za tukio hilo kutoka kwenye chumba cha marubani wa ndege ya upelelezi ya Marekani zilionyesha ndege hiyo ikitikisika mara baada ya ndege hiyo ya kivita ya China kuruka katika njia yake.

Taarifa hiyo ilisema kuwa ndege ya upelelezi ya RC-135 ilikuwa ikifanya operesheni salama na za kawaida kwenye Bahari ya South China katika anga ya kimataifa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG