Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:22

China na Russia wakamilisha zoezi la pamoja la kijeshi


Mazoezi ya kijeshi kati ya China na Russia.
Mazoezi ya kijeshi kati ya China na Russia.

Russia na China Jumatano wamekamilisha zoezi la pamoja la kijeshi la wiki moja kwenye bahari ya East China Sea.

Zoezi hilo la kuongeza ujuzi wa kunasa nyambizi chini ya bahari pamoja na kushambulia meli za kivita, limeonyeshwa na chombo cha habari cha serikali ya China cha CCTV.

Kati ya Decemba 21-27, mazoezi yaliyopewa jina Maritime Interaction-2022 yalijumuisha kikosi cha Russia cha Pacific, yaliyofanyika kwenye bahari ya karibu na Zhoushan na Taizhou katika jimbo la Zhejiang, kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la China la Xinhua.

Russia ambayo wakati mmoja ilikuwa kiongozi wa mataifa ya kikomunisti, ilishuka hadhi 1991 baada ya kuanguka kwa Umoja wa Sovieti, sasa hivi ikiwa chini ya China ambayo imepiga hatua kubwa kiteknolojia kwenye karne ya 21.

Mtu mmoja amekufa nchini China kwenye ajali iliyohusisha msongamano wa mamia ya magari kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CCTV ambalo pia limeonyesha picha za ajali hiyo iliyotokea mapema leo.

Picha zilizochukuliwa kwa ndege zimeonyesha mamia ya magari ya kila aina yakiwa yamerundikana kwenye sehemu moja ya barabara kuu iliyofunikwa na ukungu. Taarifa zimeongeza kusema kwamba takriban gari 200 zilihusika kwenye ajali hiyo karibu na mji wa Zhenghou, katika jimbo la Henan.

Ukungu mwingi ulijikusanya nyakati za asubuhi kwenye daraja la mto wa Yellow mjini humo, na kusababisha msongamano mkubwa wa magari uliopelekea ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG