Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:57

Bunge la Tanzania laidhinisha Mageuzi ya sheria za Uchaguzi


Rais Tanzania Samia Suluhu akiwa Dodoma tarehe 22 Aprili , 2021. Picha na AFP.
Rais Tanzania Samia Suluhu akiwa Dodoma tarehe 22 Aprili , 2021. Picha na AFP.

Wabunge nchini Tanzania siku ya Ijumaa wameidhinisha mageuzi ya sheria za uchaguzi licha ya malalamiko ya chama kikuu cha Upinzani cha Chadema ambacho kimeapa kuipinga sheria hiyo.

Chadema imesema miswaada mitatu hazungumzii matatizo yaliyojitokeza katika uchaguzi wa Rais uliopita wa mwaka 2020, ambapo aliyekuwa kiongozi wa kimabavu John Magufuli alishinda kwa kishindo licha ya upinzani kudai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu.

Lakini serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alichukua madaraka baada ya kifo cha Magufuli mwaka 2021 inasisitiza kufanya mageuzi yatakayo boresha demokrasia katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Maelfu ya watu walijiunga fkatika maandamano ya hivi karibuni yaliyoandaliwa na ha Chadema, ambacho kiliisihi serikali kuondoa miswaada hiyo, na kutoa wito wa uhuru zaidi kwa tume ya uchaguzi.

Bunge la Tanzania, Dodoma
Bunge la Tanzania, Dodoma

Wabunge walianza mjadala wa miswaada hiyo siku ya Jumanne kabla ya kuipigia kura Ijumaa.

“Tumefanya kazi yetu ya kuipitisha miswaada …na sasa tutaipeleka miswaada hii kwa rais kwa ajili ya kuiidhinisha na kuwa sheria” alisema spika ya bunge Tulia Ackson.

Chadema ikimelenga ukosoaji wake hususani katika hatua ambayo itamruhusu Rais Samia kufanya uteuzi wa moja kwa moja wa wajumbe watano kati ya kumi wa tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa rais wa mwakani.

Bunge la Tanzania linatawaliwa na chama tawala cha CCM ambacho kina viti 364 kati ya 392.

Maandamano ya Chadema yaliyofanyika katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam yalikuwa makubwa sana tangu serikali ilipoondoa kizuizi kwa vyama vya upinzani kufanya mikutano ya kisiasa mwaka jana.

Chanzo cha habari nii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG