Pele, mchezaji mashuhuri wa soka wa Brazil aliyeondoka kwenye umaskini wa kutembea bila ya viatu hadi kuwa mmoja wa wanasoka wakubwa na mashuhuri wanaojulikana sana katika historia. Kifo cha mwanasoka huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa mchezaji kilithibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram. Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi. Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara.
Matukio
-
Desemba 24, 2024
Waandishi wa habari Msumbiji wanavyopambana taarifa za uongo
-
Desemba 23, 2024
Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara
-
Desemba 20, 2024
Habari Potofu: MISA inawasaidia waandishi Malawi kujenga uaminifu
-
Juni 11, 2024
Je mtu yeyote anaweza kuwa rais wa Marekani?