Pele, mchezaji mashuhuri wa soka wa Brazil aliyeondoka kwenye umaskini wa kutembea bila ya viatu hadi kuwa mmoja wa wanasoka wakubwa na mashuhuri wanaojulikana sana katika historia. Kifo cha mwanasoka huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa mchezaji kilithibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram. Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi. Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara.
Matukio
-
Machi 14, 2025
Changamoto za ulezi wa watoto walemavu kiakili Kenya
-
Februari 28, 2025
Waislamu wajitayarish kwa Ramadhani
-
Februari 27, 2025
Ethiopia na Somalia waimarisha uhusiano wao
-
Februari 18, 2025
Nini kilichosababisha Raila Odinga kushindwa katika uchaguzi wa AU?
-
Februari 11, 2025
Naibu Katibu Mkuu aeleza hatua za dharura zinazochukuliwa DRC