Wine, mwanamuziki maarufu aliyegeuka kuwa mwanasiasa aliyeshindana na Rais mkongwe Yoweri Museveni katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021 nchini Uganda, amekuwa akikamatwa mara nyingi.
"Walinikamata kinyume cha sheria kama ulivyoona, na tunapozungumza hivi sasa niko chini ya kizuizi cha nyumbani. Wanajeshi na polisi wako kila mahali," Wine aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake kaskazini mwa mji mkuu Kampala.
"Mara tu nilpotua wahuni walinikamata, waliniburuza, walinikunja mikono yangu na kunifungia kwenye gari binafsi lililokuwa likisubiri.
Walinieleka hadi kwenye uwanja wa ndege wa zamani ambako walinitoa na kuniweka kwenye gari la kijeshi lililokuwa na wanajeshi wengi na maafisa wa polisi.
"Ilikuwa inadhalilisha sana," alisema Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi.
Bobi Wine pia amesema kuwa wafuasi wake 300 wamekamatwa, lakini hakutoa maelezo zaidi na AFP haikuweza kpata uthibitisho huru.
Polisi walikanusha kuwa Wine alikamatwa, walisema walikuwa "walimsindikiza" kijana huyo mwenye umri wa miaka 41 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe kwenda nyumbani kwake.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP
Forum